Majukumu ya Taasisi

Sheria namba 24 ya mwaka 1995 imeipa Taasisi majukumu makuu ya msingi ambayo ni pamoja na:-

(a) Kushauri Serikali, Mashule na Wadau mbalimbali kuhusu masuala ya chakula na lishe;

(b) Kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa chakula bora na athari za utapiamlo;

(c) Kuushawishi umma kutumia mbinu zinazoshauriwa na Taasisi katika kupambana na utapiamlo;

(d) Kutoa huduma na mafunzo katika masuala yote yanayohusiana na chakula na lishe kwenye Taasisi mbalimbali na jamii kwa ujumla;

(e) Kushiriki katika kuidhinisha vyeti vinavyotolewa katika fani ya chakula na lishe katika Jamhuri ya Muungano;

(f) Kushirikiana na Wizara na Ofisi za Mikoa na Halmashauri zinazoshughulikia mipango ya maendeleo ili kuhakikisha kwamba mipango ya kitaifa ya maendeleo inajumuisha malengo ya chakula na lishe;

(g) Kushirikiana na wazalishaji, watengenezaji na wagawaji wa chakula ili kuhakikisha kwamba chakula kinachouzwa nchini na kusafirishwa nchi za nje ni bora na salama;

(h) Kupanga na kuanzisha programu za chakula na lishe kwa manufaa ya Watanzania;

(i) Kutathmini na kufanya marekebisho ya programu za chakula na lishe;

(j) Kufanya utafiti unaohusiana na chakula na lishe; na

(k) Kutoa matokeo ya tafiti za Taasisi zinaohusu masuala ya chakula na lishe kwa Serikali na wananchi

Kutokana na majukumu hayo ni dhahiri kwamba Taasisi ina wajibu mkubwa kwenye masuala ya chakula na lishe, lengo likiwa ni kudhibiti na kutokomeza kabisa matatizo ya utapiamlo hapa nchini.