Teknolojia Habari na Mawasiliano

Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hufanya kazi katika kuhakikisha kuwa miundombinu na uwezo wa TEHAMA vinatumika vizuri na zinahusiana na malengo ya kimkakati ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania.
Malengo ya Kitengo cha TEHAMA ni:

  • Kutoa utaalam na huduma juu ya utumiaji wa TEHAMA katika Taasisi.
  • Kuboresha na kuimarisha shughuli na huduma za TEHAMA ili kukidhi mahitaji kwa wadau wa ndani na nje.

Majukumu ya Kitengo cha TEHAMA :

i.Kuhakikisha vifaa vya TEHAMA na programu zinatunzwa vizuri;
ii.Kuanzisha na kuratibu utumiaji wa mawasiliano ya barua pepe katika Mtandao;
iii.Kuratibu utekelezaji wa kubuni na kuendeleza matumizi ya tovuti ya Taasisi;
iv.Toa msaada juu ya ununuzi kulingana na programu na vifaa vya TEHAMA katika Taasisi;
v.Kusimamia mifumo ya taarifa, kanzidata, na maendeleo ya miundombinu ya mtandao.
vi.Kufanya ukaguzi wa usimamizi wa viashiria hatari na udhibiti unaohusu miundombinu ya TEHAMA na mifumo ya usimamizi ya taarifa.
vii.Kuhakikisha utekelezaji wa mifumo na shughuli za TEHAMA kulingana na Sera ya mtandao ya Serikali(e-Government policy);