Usimamizi wa Ununuzi

Utangulizi

  • Kitengo hiki kina lengo la kuleta ufanisi na kutoa huduma kwenye nyanja za ununuzi, utunzaji na usambazaji wa bidhaa na huduma mbalimbali zinazohitajika kwa ajili ya Taasisi. Kitengo hiki kinaongozwa na Afisa Ununuzi Mkuu ambaye anawajibika kwa Mkurugenzi Mtendaji.
  • Kitengo cha Ununuzi kinatekeleza majukumu yake ya ununuzi na ugavi katika Taasisi kwa mujibu wa sheria ya ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2013 na marekebisho yake ya mwaka 2016.


Majukumu ya Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi ni kama yafuatayo:

i.Kusimamia ununuzi wowote na uuzaji wa mali za Taasisi kwa njia ya Zabuni isipokuwa usuluhishi na kutunuku zabuni;
ii.Kuratibu shughuli za Bodi ya Zabuni ya Taasisi;
iii.Kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Zabuni ya Taasisi;
iv.Kufanya kazi kama Sekritarieti ya Bodi ya Zabuni ya Taasisi
v.Kuandaa mpango wa Ununuzi na Uuzaji wa mali za Taasisi kwa njia ya Zabuni;
vi.Kupendekeza ununuzi na uondoshaji wa mali za Taasisi kwa utaratibu wa Zabuni;
vii.Kukagua na kuainisha upungufu wa mahitaji katika Taasisi na kutoa tamko kuhusu mahitaji hayo;
viii.Kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili wazabuni kushiriki;
ix.Kuandaa matangazo ya fursa za zabuni;
x.Kuandaa rasimu za Mikataba;
xi.Kutoa mikataba iliyothibitishwa na kusainiwa;
xii.Kuandaa na kuhifadhi kumbukumbu za mchakato wa ununuzi na uuzaji wa mali za Taasisi;
xiii.Kuandaa na kutunza orodha au kitabu cha mikataba yote ambayo Taasisi imetunuku;
xiv.Kuandaa taarifa za kila mwezi kwa ajili ya Bodi ya Zabuni ya Taasisi;
xv.Kuandaa taarifa ya kila robo ya mwaka juu ya utekelezaji wa mpango wa ununuzi na kuwasilisha katika kikao cha menejimenti ya Taasisi;
xvi.Kufuatilia na kuhakikisha michakato ya ununuzi na taratibu zake zinafuatwa kwa mujibu wa sheria ya ununuzi wa umma;
xvii.Kuratibu kazi za ununuzi na uondoshaji wa mali za serikali katika Idara na vitengo vyote vya Taasisi;
xviii.Kuandaa taarifa nyinginezo kadri zitakavyo hitajika muda wowote;.
xix.Kushauri uongozi juu ya masuala yanayohusiana na ununuzi wa bidhaa na huduma na mchakato mzima wa kusimamia na kudhibiti mwenendo wa bidhaa na huduma katika Taasisi.;
xx.Kuhakikisha kunakuwepo na utunzaji, uhifadhi sahihi na usambazaji wa mahitaji ya ofisi wa kutosheleza na kwa wakati; na
xxi.Kutunza na Kuboresha kumbukumbu ya vifaa na rasilimali za serikali/za ofisi.