Kongamano la kimataifa la kilimo na lishe nchini Tanzania

News Image

Imewekwa: 25th Jun, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt.Germana Leyna (kulia) ameshirki kongamano la kimataifa la kilimo na lishe lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Shule ya Lishe na Tiba za magoniwa ya kitropiki ya London na wadau wengine, ambapo Wanasayansi, watunga sera, wakulima na wataalamu zaidi ya 1500 wanashiriki kwenye kongamano hilo ambalo litafanyika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 22 - 26 Juni 2025.

Katika kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kupambana na changamoto za utapiamlo nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna ameshiriki kikao cha kupitia matokeo ya utafiti wa soko la lishe “Market Assessment Survey 2025” kwa mwaka 2025.

Utafiti huo ulilenga kuangalia uelewa wa masuala ya lishe na mikakati waliyonayo katika kuimarisha lishe za wateja wao kwa makampuni yanayozalisha bidhaa za chakula na vinywaji (Food and Beverage Industry).

Mh Neema Lugangira (Mb) na Mwenyekiti mwenza wa Jukwaa la Vuguvugu la Lishe Duniani (Scaling up nutrition) akitoa neno la namna ya kutafsiri matokeo ya utafiti huu kwa vitendo.