Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

• Chumvi inapotumika kwa kiasi kidogo haina madhara
• Kwa wastani tunahitaji chini ya gramu 5(kijiko cha chai) kwa siku
• Matumizi ya chumvi nyingi yanaongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu
• Shinikizo kubwa la damu huongezeka uwezekano wa kupata magonjwa mengine kama figo,moyo na pia ya mifupa
• Ulaji wa matunda halisi una faida Zaidi ukilinganisha na juisi ya matunda
• Matunda halisi huupatia mwili vitamini pamoja na nyuzinyuzi za makapimlo
• Juisi ya matunda halisi huupatia mwili vitamini
• Makapimlo yaliyo kwenye matunda halisi husaidia kupunguza uwezekano wa kuugua saratani ya utumbo
Asusa ni kiasi kidogo cha chakula ambacho sio mlo kamili, kinachoweza kuliwa bila ya matayarisho makubwa.
Mara nyingi huliwa kati ya mlo mmoja na mwengine. Mambo yakuzingatia wakati wa kuchagua asusa:
• Chagua asusa zenye virutubisho muhimu mfano:matunda , vyakula vilivyochemshwa au kuchomwa nk.
• Epuka asusa ambazo:
 Zimekaangwa mfano:chipsi nk.
 Zinasukari nyingi mfano:keki nk
 Zenye chumvi nyingi mfano:bisi nk.
• Matumizi ya ndimu na limau hayasababishi upungufu wa damu mwilini
• Ndimu na limau ni matunda yenye vitamini C kwa wingi ambayo husaidia ufyonzwaji wa madini chuma yanayopatikana kwenye vyakula
• Madini chuma ni muhimu katika kutengeneza chembechembe nyekundu za damu
• Unaweza kutumia limau/ndimu kwa kuweka kwenye chakula au maji au kwa kuyala yenyewe
• Sio kweli kwamba mtu mwenye UKIMWI haruhusiwi kutumia sukari,kila mtu anashauriwa kutumia kiasi kidogo cha sukari
• Sukari ni chanzo kimojawapo cha nishati ambayo huupatia mwili nguvu na joto
• Wanaoishi na VVU na wenye UKIMWI wanapokuwa na fangasi kinywani au kooni wanashauriwa kupunguza matumizi ya sukari ili kutokuchochea kukua kwa fangasi
• Matumzi ya sukari yanaweza kuendelea baada ya fangasi kupona
• Asali ina nishati kwa wingi
• Asali ina virutubishi kama utomwili(protein) vitamini na madini
• Asali hufanya kazi ya kiuavijasumu(antibiotic) hivyo huweza kutumika katika kutibu kikohozi,fangasi kinywani na vidonda vya mdomoni na kooni
• Hata hivyo inashauriwa kusukutua kinywa mara baada ya kula asali ili kuondoa mabaki ya sukari yanayoweza kuleta madhara kinywani
• Kitunguu saumu kina uwezo wa kuua bacteria ,virusi na fangasi hususani katika matumbo,mapafu na ukeni
• Husaidia kutibu utando kinywani,maambukizi katika koo,malengelenge kwenye ngozi na kuharisha
• Kitunguu saumu pia husaidia umeng’enywaji wa chakula tumboni
• Mtindi humeng’enywa kwa urahisi Zaidi mwilini ikilinganishwa na maziwa mabichi(fresh)
• Pia mtindi husaidia umeng’enywaji na ufyonzwaji wa virutubishi vinavyopatikana kwenye vyakula vingine
• Watu wanaoishi na VVU hupata matatizo ya umeng’enywaji na ufyonzwaji wa virutubishi mwilini,hivyo mtindi unakuwa faida kwao
• Watu wenye uzito mkubwa kupita kiasi huwa na hatari Zaidi ya kupata matatizo ya moyo,shinikizo la damu na ugonjwa wa kisukari
• Mtu anayeishi na VVU au mwenye UKIMWI anashauriwa awe na uzito wa kadiri- si mkubwa sana wala si mdogo sana
• Ufafanuzi wa uzito wa kadiri unaweza kutolewa na wataalam wa afya au wa lishe
• Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI au wenye UKIMWI na magonjwa mengine hawashauriwi kunywa pombe.
• Pombe humfanya mtu kokosa hamu ya kula na pia huingilia mchakato wa metaboli mwilini
• Unywaji wa pombe hufanya ini kuharibika hivyo kushindwa kufanya kazi yake ya kuondoa sumu mbalimbali mwilini
• Pombe pia huingilia mfumo wa fahamu na hivyo kupunguza uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kama vile ngono salama