Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe

Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe ni mojawapo ya idara tano za Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania. Idara hii ina majukumu yafuatayo:

 • Kuandaa na kupitia mitaala na miongozo ya mafunzo ya chakula na lishe kwa kushirikiana na taasisi husika.
 • Kusimamia na kuboresha maktaba ya kitaifa ya lishe.
 • Kuratibu uandaaji na utoaji wa taarifa za chakula na lishe kwa umma
 • Kufanya tafiti katika elimu na mafunzo ya chakula na lishe.
 • Kuratibu na kuendesha mafunzo kazini ya chakula na lishe kwa watumishi wa Taasisi na watoa huduma wengine.

Idara ina vitengo vinne ambavyo ni mawasiliano serikalini, mafunzo ya lishe kwa watendaji walio kazini, maktaba ya chakula na lishe na uchapishaji. Vitengo hivi vinamajukumu yafuatayo:

1.Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

 • Kuratibu utoaji wa elimu ya lishe kwa umma kwa kupitia vyombo vya habari ambavyo ni pamoja na redio, runinga, magazeti, vipeperushi, mabango, video, mitandao ya kijamii (twitter, facebook, instagram, blog) na tovuti ya Taasisi.
 • Kuandaa na kusambaza machapisho mbalimbali ya masuala ya lishe
 • Kuandaa na kusambaza jumbe muhimu zinazotokana na tafiti za chakula na lishe.
 • Kuratibu kumbukumbu, maadhimisho, maonesho na kampeni za chakula na lishe
 • Kufanya tafiti zinazohusu mawasiliano yanayolenga mabadiliko ya tabia zinazoathiri lishe ya jamii.

2.Kitengo cha mafunzo ya lishe kwa watendaji walio kazini

 • Kuratibu mafunzo ya chakula na lishe kwa watendaji wa sekta mbalimbali, asasi za kiraia na wadau wengine.
 • Kuandaa miongozo na vitini vya mafunzo ya chakula na lishe.
 • Kushauri taasisi mbalimbali za elimu na mafunzo kuingiza masuala ya lishe katika mitaala yao.
 • Kufanya tathimini kuhusu mahitaji ya mafunzo ya chakula na lishe kwa watendaji wa sekta mbalimbali, asasi za kiraia na wadau.

3.Kitengo cha Maktaba ya Chakula na Lishe

 • Kutafuta taarifa za tafiti na machapisho mengine yanayohusu chakula na lishe kutoka vyanzo mbalimbali.
 • Kutunza machapisho yanayohusu masuala ya chakula na lishe.
 • Kuwasaidia watumiaji wa maktaba kupata taarifa za masuala ya chakula na lishe.
 • KUHUSU MAKTABA BONYEZA HAPA

4.Kitengo cha Uchapishaji

 • Kuchapisha machapisho mbalimbali.

MIRADI /PROGRAMU

 • Lishe ya Watoto Wachanga na Wadogo,Wanawake Wajawazito na Wanaonyonyesha na Vijana Balehe
 • Mkoba wa Siku 1000 wa Mawasiliano yenye Kulenga Mabadiliko ya Tabia
 • Matumizi ya Virutubishi Mchanganyiko (Vitamini na Madini) kwa Watoto kuanzia umri wa miezi Sita(6)Mpakaumri wa Miaka Mitano(5)
 • Lishe mashuleni
 • Mawasiliano ya Umma na Machapisho
 • Maktaba
 • Upitiaji na uendelezaji wa mitaala ya Chakula na Lishe