Ushiriki wa Sekta Binafsi katika kupambana na changamoto za Utapiamlo.

News Image

Imewekwa: 29th Jun, 2025

Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bw. Obey Assery (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti mwenza wa Jukwaa la Vuguvugu la Lishe Duniani (Scaling up nutrition Movement) Mhe. Neema Lugangira (wa pili kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa TFNC Dkt. Germana Leyna (wa kwanza kulia) pamoja na Bi. Bo-Jane Woods kutoka ATNi (Access to Nutrition initiative) mara baada ya kushiriki kikao cha kupitia matokeo ya utafiti wa soko la lishe “Market Assessment Survey 2025” kwa mwaka 2025.

Utafiti huo ulilenga kuangalia uelewa wa masuala ya lishe na mikakati waliyonayo katika kuimarisha lishe za wateja wao kwa makampuni yanayozalisha bidhaa za chakula na vinywaji (Food and Beverage Industry).