TAMISEMI  YAIUNGA MKONO TFNC KUELEKEA  UTEKELEZAJI WA MRADI WA IMAN AWAMU YA PILI
16 Jun, 2026
TAMISEMI  YAIUNGA MKONO TFNC KUELEKEA  UTEKELEZAJI WA MRADI WA IMAN AWAMU YA PILI
Dodoma, Juni 12, 2026   Timu ya wataalamu kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) pamoja na wadau wa Mradi wa IMAN II (Lishe Yangu), leo imekutana na viongozi wa Ofisi ya Waziri – TAMISEMI mjini Dodoma kwa lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa mradi huo unaolenga kuboresha lishe kwa wanawake wajawazito nchini.   Kikao hicho kimeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Dkt. Paul Chaote , na kuhudhuriwa na Wataalamu kutoka  Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wakiongozwa na Msimamizi wa Shughuli za Lishe nchini kutoka Shirika hilo Bwa. Patrick Codjia na maafisa wengine kutoka TAMISEMi.   Katika kikao hicho, washiriki wamejadili hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi, ikiwa ni pamoja na maandalizi ya uzinduzi rasmi wa IMAN II na namna ya kuwafikia walengwa ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi.   Dkt Chaote amesisitiza  ushirikiano wa karibu kati ya TFNC, TAMISEMI na UNICEF katika utekelezaji wa mradi huo  ili kuleta matokeo chanya yatakayosaidia kuboresha afya na lishe ya wanawake wajawazito nchini.     Uzinduzi rasmi wa mradi huo unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni, 2026 katika Mkoa wa Njombe, ambapo wadau mbalimbali wa sekta ya afya na lishe wanatarajiwa kushiriki.