Idara ya Fedha, Utumishi na Utawala

Idara ya Fedha, Utumishi na Utawala ni miongoni mwa Idara tano za Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania. Idara hii ina vitengo vitatu ambavyo ni : Uhasibu, Utumishi na Utawala. Kimsingi majukumu ya Idara yamejikita katikavitengo hivyo:

Majukumu yaIdara yaFedha Utumishi na Utawala

i.Kuratibu kazi za kila siku za vitengo vya Uhasibu, Utumishi na Utawala.

ii.Kuhakikisha taarifa za Fedha kila mwezi, robo mwaka na Hesabu za mwisho za Taasisi zinaandaliwa.

iii.Kushauri na kuratibu shughuli mbalimbali za kuiongezea Taasisi Mapato (income generating activities)

iv.Kwa kushirikiana na Mkuu wa Idara ya Mipango na sera ya Lishe kuaandampango wa Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Taasisi kwa mwaka

v.Kufanya kazi mbalimbali kama atakavyo pangiwa na Mkurugenzi Mtendaji

Majukumu ya Vitengo:

Utumishi:

 • Kuandaa na kulipa mishahara ya watumishi kila mwezi
 • Kuandaa na kusimamia mchakato wa ajira mpya.
 • Kuingizana kufuta taarifa mbalimbaliza kiutumishi kwenye mfumo wa mishahara(Lawson)
 • Kuratibu ujazaji na mapitio ya Opras kwa watumishi
 • Kuwasiliana na Idara Kuu ya Utumishi juu ya masuala mbalimbali ya kiutumishi.

Utawala:

 • Uboreshaji wa masijala ya Taasisi.
 • Kusimamia shughuli za usafi wa majengo na mazingira ya Taasisi.
 • Kusimamia ukarabati mdogo kwenye majengo ya Taasisi.
 • Kuhakikisha vitendea kazi kama vile kompyuta, fotokopi na viyoyozi vipo kwenye hali nzuri.
 • Kusimamia ulinzi wa Taasisi
 • Kushughulikia barua na nyaraka mbalimbali zinazoingia na kutokanje ya Taasisi

Uhasibu:

 • Uandaaji wa hesabu za mwisho za Taasisi kwa kila mwisho wamwaka wa Fedha
 • Kushiriki katika ukaguzi wa hesabu za mwisho kwa kilamwaka wa Fedha
 • Kujibu hoja za ukaguzi zinazotolewa na mkaguzi wa ndani na mkaguzi wa nje.
 • Kufanya usuluhisho wa kibenki kwa akaunti za Taasisi kila mwezi.
 • Kuandaa Taarifa zaMapato na Matumizikila mwezina robo mwaka
 • Kufanya malipo mbalimbali ya Taasisiya kila siku
 • Kufuatilia mapokezi ya Fedhaza Mapato ya ndani
 • matumizi mengineyo (OC) na fedha za makato ya Mishahara Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto.
 • Kufuatilia uhakiki wa madeni ya Taasisi kwa Msajili wa Hazina nakwa Katibu Mkuu - Hazina