Maadhimisho ya wiki ya unyenyeshaji duniani 2025

News Image

Imewekwa: 8th Aug, 2025

Mkurugenzi Idara ya Elimu na Mafunzo,Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania(TFNC), Dkt. Esther Nkuba akifanya mahojiano na watangazaji wa TBC One kipindi cha jambo kuelezea umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji tarehe 07 Agosti, 2025.

Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki ipasavyo katika kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Thamini Unyonyeshaji; weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoro".

Afisa Lishe Mtafiti, Fatma Juma kutoka TFNC akitoa elimu ya unyonyeshaji kwa akina mama waliofika kupata huduma katika kituo cha afya Kibada Kigamboni ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji inayoadhimishwa kila mwaka 1-7 Agosti.

Maadhimisho ya mwaka huu yanaenda na kauli mbiu inayosema "Thamini Unyonyeshaji; Weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto"

Afisa Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Josephine Manase akiongea na wazazi/walezi kuhusu umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto wakati wa sherehe za kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni iliyofanyika katika kituo cha Afya Kigamboni jijiji Dar es salaam.

Afisa Lishe Mtafiti, Nusura Salumu kutoka TFNC akitoa elimu ya unyonyeshaji kwa akina mama waliojifungua katika wodi ya wazazi kituo cha afya Kibada Kigamboni ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji inayoadhimishwa kila mwaka 1-7 Agosti. Maadhimisho ya mwaka huu yanaenda na kauli mbiu inayosema "Thamini Unyonyeshaji; Weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto"

Afisa Lishe Mtafiti, Elizabeth Lyimo(picha ya mkono wa kushoto) na Afisa Lishe Mtafiti Juma Mbaruku(picha ya mkono wa kulia) kutoka TFNC wakitoa elimu juu ya umuhimu wa unyonyeshaji maziwa ya mama katika wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama katika kituo cha Afya cha Kawe ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji inayoadhimishwa kila mwaka 1-7 Agosti. Maadhimisho ya mwaka huu yanaenda na kauli mbiu inayosema "Thamini Unyonyeshaji; Weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto"