24 Feb, 2026
Mwalimu wa Lishe Shule ya Msingi Unubini, iliyopo Manispaa ya Temeke, Mwl. Ramadhani Nurdin akiwafundisha wanafunzi wa klabu ya Afya na Lishe kuhusu Mlo Kamili wakati wa zoezi la kutoa ushauri wa kitaalamu wa uendeshaji na usimamizi wa klabu hizo(Picha ya kwanza kushoto).
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Unubini, iliyopo Manispaa ya Temeke, wakijibu maswali kuhusu dhana ya mlo kamili wakati wa kipindi cha klabu ya Afya na Lishe(Picha ya pili kushoto).
Shule ya Unubini ni moja ya shule 15 za msingi Manispaa ya Temeke zilizo chini ya Mradi wa Afya na Lishe unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Manispaa ya Temeke na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).
