24 Feb, 2026
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Unubini, iliyopo Manispaa ya Temeke, wakijibu maswali kuhusu dhana ya mlo kamili wakati wa kipindi cha klabu ya Afya na Lishe. (Picha ya kwanza kushoto).
Afisa Elimu Watu Wazima Manispaa ya Temeke, Sister, Mwl. Donasiana Njuu akiwaonesha wanafunzi wa shule ya msingi Unubini, kitabu cha Lishe Yangu, Afya Yangu kilichobuniwa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)(Picha ya pili kulia).
Shule ya Unubini ni moja ya shule 15 za msingi Manispaa ya Temeke zilizo chini ya Mradi wa Afya na Lishe unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Manispaa ya Temeke na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)
