Je, ni kweli kwamba ndimu na limau hupunguza damu mwilini?
Kumekuwa na dhana potofu kwa watu wengi juu ya faida na matumizi ya ndimu na limau kilishe, wengu huamini kwamba matumizi ya ndimu na limau si mazuri kwa sababu yanasababisha upungufu wa damu, jambo ambalo si kweli.
Ndimu na limau ni matunda yenye vitamini C ambayo husaidia katika ufyonzwaji wa madini ya chuma yanayopatikana kwenye vyakula. Madini ya chuma ni muhimu katika kutengeneza chembechembe nyekundu za damu. Kwa mantiki hiyo matumizi ya ndimu na limau hutumika kama kichocheo kimajawapo cha kuongeza damu mwilini na wala si kupunguza damu mwilini.
Pia ifahamike kwamba ndimu na limau husaidia kuongeza hamu ya kula hasa kwa mtu anayepata kichefuchefu na kutapika.