Kikao kuhusu masuala ya lishe na Mhe. Dkt. Rajabu Rutengwa, Mkuu wa Mkoa Mstaafu
Imewekwa: 16th Dec, 2025
Mhe. Dkt. Rajabu Rutengwa, Mkuu wa Mkoa Mstaafu Katavi, Tanga na Morogoro (wa kwanza kulia) akiwa na wajumbe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji (wa pili kulia) Dkt. Germana Leyna wakijadili namna TFNC inavyoweza kujenga uwezo na kuongezeka ufanisi wa wataalamu wa sekta mtambuka katika kutekeleza Mkakati Jumuishi wa Lishe wa pili (NMNAP II ) katika ngazi za Mikoa na Halmashauri. Majadiliano hayo yamefanyika 11 Desemba, 2025 katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa TFNC.
