Zoezi la kukusanya taarifa katika utafiti wa kuhakiki ufanisi wa unga mchanganyiko wa mbegu za mchicha

News Image

Imewekwa: 8th Jan, 2026

Mkurugenzi Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dkt. Esther Nkuba akiongea na Watoa Huduma za Afya ngazi ya Jamii kutoka jiji la Arusha na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kuhusu mradi wa kupambana na utapiamlo wa kati kwa kutumia mbegu za mchicha na nafaka nyingine, kabla ya kuanza kwa zoezi la kuhakiki ufanisi wa unga mchanganyiko wa mbegu za mchicha na nafaka nyingine katika kupunguza utapiamlo nchini.

Utafiti wa kuhakiki ufanisi wa unga mchanganyiko wa mbegu za mchicha na nafaka nyingine utafanyika kwa miezi sita katika Halmashauri mbili za mkoa wa Arusha (Arusha jiji na Arusha Vijijini).