MAFUNZO KWA WATAALAMU WA MAABARA.

News Image

Imewekwa: 16th Dec, 2025

Wafanyakazi wa Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), wamepatiwa mafunzo ya kanuni bora za ufanyaji Kazi kwenye maabara yaani GLP na GCLP, ikiwa ni sehemu ya kuboresha usimamizi, ubora na usalama katika Maabara ya Chakula na Lishe iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yametolewa na mwezeshaji Prof. Reginad Kavishe kutoka KCMC University na yamefanyika mkoani Morogoro katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine.