Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

• Inashauriwa kuwa watu wanywe maji kwa wingi,angalau lita moja na nusu kwa siku

• Maji husaidi katika uyeyushwaji wa chakula na usafirishaji wa virutubishi mwilini

• Maji pia husaidia kuondoa uchafu na kemikali zisizotakiwa mwilini

• Vinywaji vingine vinavyochangia kuongeza maji mwilini ni pamoja na juisi ya matunda, madafu,maziwa,supu n.k.
• Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI anaweza kutumia pilipili katika vyakula na vinywaji mbalimbali

• Hata hivyo, inashauriwa pilipili itumike kwa kiasi kidogo

• Iwapo mtu mwenye virusi vya UKIMWI anavidonda mdomoni au kooni,au ikiwa anaharisha,anashauriwa asitumie pilipili kabisa

• Pilipili huzidisha maumivu ya vidonda na pia,kutokana na mwasho wake,husababisha usumbufu tumboni hivyo kuzidisha hali ya kuharisha