Kikao cha Majadiliano ya Kitaifa cha Wataalamu kuhusu utekelezaji wa ahadi ya N4G
01 Mar, 2026
Kikao cha Majadiliano ya Kitaifa cha Wataalamu kuhusu utekelezaji wa ahadi ya N4G
Ofisi ya Waziri Mkuu imesisitiza umuhimu wa kuwa na mfumo madhubuti wa utekelezaji na uwajibikaji katika kufikia ahadi ya Lishe kwa Maendeleo ( N4G). Akifungua kikao cha Majadiliano ya Kitaifa cha Wataalamu kuhusu utekelezaji wa ahadi ya N4G, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali, Bw. Omar Ilyas, ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (SBUU) Dkt. Jim Yonazi, alisema kuwa ili kufikia malengo ya N4G, ni muhimu kuwa na mfumo unaotekeleza ahadi hiyo kwa ufanisi na unaozingatia uwajibikaji. “Kwa ajili ya utekelezaji wa ahadi ya Lishe kwa Maendeleo, ni lazima tuwe na mfumo wa utekelezaji ulio wazi, uliothibitishwa kitaalam, na wa kutoa taarifa kwa wakati unaofaa,” alisema Bw. Ilyas. Alisisitiza pia kuwa, ufanisi wa ahadi hii unahitaji ushirikiano wa pande mbalimbali, ikiwa ni pamoja na serikali, mashirika ya kimataifa, na jamii kwa ujumla.