Kampeni ya matone ya Vitamini A

News Image

Imewekwa: 24th Jun, 2025

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Otilia Gowele akimpatia mtoto kidonge cha vitamini A katika zahanati ya Kijitonyama wakati wa ziara ya kukagua zoezi la kampeni ya utoaji wa vidonge vya vitamini A na dawa za minyoo zinazotolewa bure nchi nzima kwa watoto wenye umri wa miezi 6-59.

Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Emily Burn akishiriki kampeni ya utoaji wa vidonge vya vitamini A na dawa za minyoo katika zahanati ya Kijitonyama wakati wa ziara ya kukagua zoezi hilo linalotekelezwa nchi nzima kwa watoto wenye umri wa miezi 6-59.

Mkurugenzi Mkazi wa shirika la kimataifa la Nutrition International (NI) nchini Tanzania Dr. George Mwita akiongea na wananchi katika zahanati ya Kijitonyama kuhusu ushiriki wa NI kupitia ufadhili wa Canada katika utekelezaji wa kampeni ya utoaji wa matone ya vitamini A bure kwa watoto wote nchini wenye umri wa miezi 6-59