Taasisi ya Chakula na Lishe amepokea sampuli za chumvi kwa ajili ya utafiti

Imewekwa: 22nd Oct, 2024
Mratibu wa programu ya kuzuia upungufu wa madini joto Bi Rose Msaki wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) akipokea sampuli za chumvi kutoka mkoa wa Singida, Ikiwa ni sehemu ya utafiti wa programu ya chumvi (USI) unaolenga kuangalia uwezekano wa kutumia mfumo wa sekta ya afya kupima kiwango cha madini joto katika chumvi na mikojo (USI surveillance System).
Kukamilika kwa utafiti huu kunatajwa utaiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za kwanza Afrika kupima hali ya viwango vya madini joto katika jamii kwa kwa wakati kwa kutumia mifumo endelevu badala ya kusubiri tafiti za kitaifa zinazofanyika kila baada ya miaka mitano.