Wadau wa Lishe wakutana kujadili changamoto za lishe nchini
Imewekwa: 20th Apr, 2021
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania yakutana na wadau wa Lishe kujadili njia zinazoweza kutatua changamoto za lishe nchini pamoja na kupitia nadharia ya mabadiliko itakayotoa mwongozo wa kuandaa awamu ya pili ya Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Lishe. Kikao hicho kimefanyika tarehe 13 hadi 15 Aprili 2021 katika ukumbi wa Protea, Dar es salaam.