Mkutano wa pamoja na watafiti wa mradi wa GROWNNUT II unafanyika nchini Afrika ya Kusini

Imewekwa: 10th Oct, 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana (wa pili kulia mstari wa nyuma) , ameshiriki Mkutano wa pamoja na watafiti wa mradi wa GROWNNUT II unaofanyika Durban nchini Afrika ya Kusini, Ukilenga kuongeza idadi ya Watalaam wa Epidemiolojia ya lishe (Nutrition Epidimiology) katika nchi za Tanzania na Jamhuri ya Kongo (DRC).
Mradi huu unatekelezwa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Skuli ya Afya ya Jamii Chuo Kikuu cha Kinshasa, Chuo Kikuu cha Kwazulu Natal na Chuo Kikuu cha Bergen kwa ufadhili wa Serikali ya Norway kupitia mpango wa NORHED.
Afisa Lishe Mtafiti Medina Wandela ni miongoni mwa watafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe waliosajiliwa katika shahada ya Uzamivu kupitia mradi huu.