Mkutano wa kikanda wa kujali Mikakati ya kupambana na upungufu wa damu

Imewekwa: 1st Aug, 2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna pamoja Meneja wa Maabara ya Taasisi Bwa.Tedson Lukindo, wameshiriki kwenye Mkutano wa kikanda wa kujali Mikakati ya kupambana na upungufu wa damu (Anaemia) unaoendelea kufanyika nchini Kenya.
Baadhi ya nchi Afrika ikiwemo Senegal, Ghana, Malawi, Burkina Faso, Nigeria, Ethiopia, Uganda, Tanzania, Rwanda na Kenya zimeshiriki katika Mkutano huo ambao umelenga kujadili changamoto za taarifa, vigezo vipya vya uchakataji taarifa na matumizi ya taarifa hizo katika kupanga na kusimamia afua na programu mtambuka.
Mkutano huo umeshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo CDC, WHO, UNICEF, BMGF, USAID Numeral, IGAD, Micronutrient Forum, DInA na Anemia Action Alliance, ambapo unatarajia kuhitimishwa Agosti 2, 2024.