MAFUNZO YA MFUMO WA MNIS KWA WATUMISHI WA TFNC

Imewekwa: 25th Jan, 2022
Wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania wakiwemo wakuu wa idara na vitengo, wakuu wa miradi wakiudhuria mafunzo ya mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa taarifa za lishe nchini (MNIS) yaliyoandaliwa na Idara ya Sera na Mipango ya Lishe kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kuujua mfumo huo, viashiria vilivyopo, utekelezaji wa viashiria hivyo kwa ngazi mbalimbali pamoja na jinsi ya kuchataka taarifa zilizopo kwenye mfumo ili kuweza kupanga bajeti za afua za lishe na kufanya maamuzi yenye ushahidi wa kisayansi.