Elimu ya lishe yatolewa kwa wanafunzi wa chuo cha IFM

Imewekwa: 11th May, 2025
Afisa Lishe Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Adeline Munuo akiwasilisha mada kuhusu ulaji unaofaa na mitindo bora ya maisha kwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), kupitia mradi wa RECAP unaosimamiwa na Wizara ya Afya.
Jumla ya wanafunzi 120 wa IFM walihudhuria kongamano hilo ambapo waliweza kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo upimaji wa afya na ushauri wa kilishe kutoka kwa wataalamu wa TFNC, TANCDA na Muhimbili