TFNC yajivunia miaka minne ya JPM

News Image

Imewekwa: 24th Jan, 2020

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imetaja mafanikio iliyoyapata katika miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa TFNC, Dkt Germana Leyna ameyataja mafanikio hayo wakati wa ziara ya maoafisa mawasiliano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, na taasisi zilizo chini yake ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya “Tumeboresha Sekta ya Afya”

“Mafanikio tuliyoyapata katika awamu hii ni pamoja na kupunguza matatizo mbalimbali ya utapiamlo nchini. Tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano lililopungua kutoka 34% mwaka 205/16 hadi 32% mwaka 2018, ukondefu uliopungua kutoka 4.5% mwaka 2015/16 hadi 3.5% mwaka 2018 na tatizo la upungufu wa damu kwa wanawake walio katika umri wa uzazi (miaka 15-49) lililopungua kutoka 45% mwaka 2015/16 hadi 29% mwaka 2018” amesema Dkt. Leyna.

Dkt. Leyna amesema TFNC imefikia mafanikio hayo kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau ikiwemo kuanzisha Mpango Jumuishi wa Lishe wa Kitaifa (NMNAP), uboreshwaji wa maabara ya lishe na sayansi ya chakula, uboreshaji wa utoaji wa elimu ya lishe kwa kuongeza mbinu ya kubadili tabia kwa kutumia "Mkoba wa siku 1000" pamoja na uendeshaji wa afua mbalimbali za lishe nchini.