KIKAO KAZI

News Image

Imewekwa: 28th Feb, 2023

Waziri wa nchi OR -TAMISEMI, Mh Anjela Kairuki ambaye ni mwenyekiti wa kazi ya Tathmini ya haraka ya visababishi vya utapiamlo katika mikoa yenye viwango vikubwa vya udumavu nchini amekutana na timu ya Big Win Philanthropy pamoja na kamati ya wataalamu kujadili hatua zilizofikiwa katika kutekeleza kazi hiyo.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu WN OR TAMISEMI, Mh Festo Dugange, Dr Germana Leyna - Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe pamoja na maafisa kutoka OR TAMISEMI na Wizara ya Afya.

Timu ya Big Win Philanthropy ikiwa katika kikao cha pamoja na Kamati ya Kitaalamu kujadili namna ya kuendesha zoezi la Tathmini ya haraka ya visababishi vya utapiamlo katika mikoa yenye viwango vikubwa vya udumavu nchini.

Zoezi hili ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan kuiwezesha nchi kushiriki kikamilifu katika Kundi la Marais Vinara wa Lishe (Presidential Dialogue Group on Nutrition).

Tathmini hii inafanyika chini ya usimamizi wa OR TAMISEMI ambapo Taasisi ya Chakula na Lishe ni Sekretariati kwa ufadhili wa Big Win Philanthropy na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Washiriki wengine wa kikao hicho wametoka Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Mkuu waMkoa wa Dodoma na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.