Mwongozo wa Chakula na Ulaji Tanzania Bara_Toleo la Kiswahili_2023

Imewekwa:Jan 26 , 2024

Mwongozo wa Chakula na Ulaji Tanzania Bara_Toleo la Kiswahili_2023 - Bonyeza hapa

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuboresha hali ya lishe na afya za watu wa rika na makundi yote katika jamii ya Watanzania. Dhamira ya kuboresha hali ya lishe na afya ya Watanzania inadhihirishwa katika sera, mikakati, mipango ya maendeleo na afua mbalimbali zinazokusudia kupunguza aina zote za utapiamlo nchini.

Kama ilivyo kwanchi nyingine zinazoendelea, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakabiliwa na aina mbalimbali zautapiamlo ambazo zinazosababisha athari katika maendeleo ya mtoto kimwili na kiakili, kupungua kwauwezo wa kujifunza, na hivyo kuathiri tija katika utendaji kazi. Ingawa Tanzania imepiga hatua katikakukabiliana na utapiamlo, ongezeko la kasi la kiwango cha uzito uliozidi na unene kupita kiasi nchini unatoa mwelekeo mpya katika mikakati ya kitaifa inayohitajika ili kukabiliana na hali hii.

Baadhi ya sababu zinazochangia utapiamlo ni pamoja na mabadiliko miongoni mwa jamii juu ya utaratibu na namna ya ulaji, na mitindo ya maisha. Katika kukabiliana na hali ya utapiamlo nchini, Wizara ya Afya, kupitia Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), imetengeneza Mwongozo wa kitaifa ya Chakula na Ulaji unaofaa kwa watu wote; isipokuwa kwa wale ambao tayari wana matatizo ya kiafya. FAO imesaidia mchakato huu kwa kutoa msaada wa kifedha na wa kitaalam.

Mwongozo huu umetayarishwa kwa kutumia mbinu shirikishi ambayo imejumuisha wataalamu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Katika kutekeleza jukumu hili, timu ya wataalam ilizoundwa ambayo pamoja na shughuli nyingine zilizotekelezwa, iliaandaa ripoti ya ushahidi ambayo imeainisha matatizo ya lishe na changamoto za ulaji tulizonazo hapa nchini na mapendekezo yametolewa ili kusaidia

uandaaji wa mwongozo huu.

Mapendekezo haya ya kiutaalam ya mwongozo wa chakula na ulaji unaofaa yatatumika kama nyaraka rasmi kuongoza juu ya ulaji na mitindo bora ya maisha yenye tija katika kuboresha hali ya lishe na mtindo bora ya maisha. Pia, mwongozo huu itakuwa nyenzo muhimu katika kuwezesha masuala yanayohusu taarifa na elimu ya chakula na lishe nchini. Mwongozo huu ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kuboresha hali ya lishe kwa kupitia

(i)Afua za lishe zinazotekelezwa na sekta mtambuka na zile zinazotekelezwa na sekta ya afya,

(ii)Mwongozo wa kuboresha upatikanaji wa madini na vitamini,

(iii)Sera inayohusu ulishaji wa watoto wachanga na wadogo, na

(iv)Mikakati ya kuongeza virutubisho kwenye chakula.

Pia, mwongozo huu ya ulaji inasaidia utekelezaji wa mpango jumuishi wa taifa wa lishe wa pili kwa mwaka 2021-2026. Aidha, tunatazamia kuwa mwongozo huu utasaidia kuimarisha uhusiano wa kiuetendaji baina ya sekta za kilimo, lishe na afya katika kusimamia masuala ya lishe nchini.

Mwongozo huu unakusudiwa kutumiwa na wataalam mbalimbali wakiwemo wataalamu wa lishe, watafiti, wadau wa maendeleo, waelimishaji lishe wa jamii, watumishi wa afya, walimu na wadau wengine wanaoboresha hali za lishe na afya za umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla.