Watafiti kutokaTaasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) pamoja na Wataalamu wa Masuala ya athari za kiafya za upungufu wa madini joto mwilini kutoka Shirika la Iodine Global Network (IGN) Tanzania, wamefanya ziara katika Mkoa wa Dar Es Salaam, Mtwara na Singida na kufanya majadiliano na kupeana maelekezo na watendaji wa ngazi za Mkoa na Halmashauri kuhusu namna ya kuendeleza utekelezaji wa utafiti wa programu ya chumvi (FORTIMAS) awamu ya pili unaolenga kuangalia uwezekano wa kutumia mfumo wa ufuatili...