Zoezi la upandaji miti katika Ofisi za Maabara ya Taasisi

Imewekwa: 2nd Feb, 2023
Menejimenti ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt.Germana Leyna wameshiriki zoezi la upandaji miti katika Ofisi za Maabara ya Taasisi zilizopo Mikocheni ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhifadhi na kutunza Mazingira. Dkt. Germana amesema takribani miti 133 ya matunda itapandwa katika eneo hilo na wamekuchukua uamuzi huo ikiwa ni kuhamasisha jamii kushiriki katika utunzaji wa mazingira na kufikiria kupanda mimea ambayo inaweza kuwasaidia kuepukana na changamoto za lishe duni |
|
|