Zoezi la kutathmini hali ya lishe kwa watoto mkoani Njombe linaendelea

News Image

Imewekwa: 19th Feb, 2024

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Njombe pamoja na Shirika la Kuhudumia Watoto duniani (UNICEF) wanaendelea na zoezi la kutathmini hali ya lishe kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 pamoja na wanawake walio katika umri wa kuzaa (miaka 15 -49) katika mkoa wa Njombe, zoezi ambalo litaenda sambamba na kuangalia visababishi mbalimbali vya tatizo la Udumavu katika mkoa huo.

Tayari timu ya Waalaamu kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, UNICEF na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, imetoa mafunzo ya wadadisi wa taarifa za lishe katika ngazi ya kaya ili kukusanya taarifa kwa ufanisi


Zoezi la ukusanyaji wa taarifa za lishe na visababishi vya tatizo la udumavu katika ngazi ya kaya linaendelea katika halmashauri zote za mkoa wa Njombe_RS; TFNC kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Njombe pamoja UNICEF wanaendelea na zoezi la kutathmini hali ya lishe kwa watoto wali chini ya umri wa miaka 5 pamoja na wanawake walio katika umri wa kuzaa (miaka 15 -49) zoezi ambalo litaenda sambamba na kuangalia visababishi mbalimbali vya tatizo la Udumavu katika mkoa huo.