​ZIARA YA MGANGA MKUU WA SERIKALI

News Image

Imewekwa: 17th Dec, 2021

MGANGA Mkuu wa Serikali Dkt. Aifillo Sichalwe kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) mara baada ya kutembelea Taasisi hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo katika kupunguza tatizo la Utapiamlo nchini.

Awali kabla ya kuzungumza na wafanyakazi hao, Dkt. Sichalwe alipata fursa ya kusikiliza maelezo kuhusu utendaji wa Taasisi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Germana Leyna na Wakurugenzi wa Idara katika Taasisi ambapo waliweza kubainisha majukumu na wajibu wa Taasisi, maendeleo ya kazi za Taasisi, miradi inayotekelezwa, changamoto na juhudi zinazochukuliwa katika kukabiliana na utapiamlo nchini.

Mganga Mkuu wa Serikali kwa upande wake alisema kwa kutambua umuhimu wa lishe Wizara itaendelea kuipa ushirikiano Taasisi hiyo ili iweze kufanikisha malengo yake ya kutoa huduma za lishe kwa wananchi. Hatahivyo, alitoa rai kwa Taasisi kutafuta namna bora zaidi ya kufikisha huduma za lishe kwa jamii na kuhakikisha kuwa zinaeleweka vizuri na kukubalika na jamii.