Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya katika Maabara ya TFNC

News Image

Imewekwa: 24th Mar, 2024

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu tarehe 22 Machi, 2024 amefanya ziara kwenye Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukagua na kuona kazi zinazofanyika katika maabara hiyo.

Maabara hiyo imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Kemia ya Chakula kwa ajili ya Uchunguzi wa Viinilishe, uchafuzi na sumu za asili mfano sumu kuvu, cyanide kwenye mihogo n.k; Biokemia kwa ajili ya Uchunguzi wa viashiria vya lishe mwilini na hali ya lishe; na mwisho ni Mikrobiologia kwa ajili ya Uchunguzi wa viashiria vya viinilishe mwilini na uchunguzi wa ubora na usalama wa chakula.