“Waheshimiwa wabunge wenzangu hili halina mjadala twendeni tukaishauri Serikali tuhakikishe wanaweka kipaumbele kwenye afua za lishe, utaendelea kutibu wananchi wengi kwa sababu ya lishe mbovu wakati lishe ni tiba namba moja tena ya bei nafuu.”Amesema Mhe. Nyongo.
Aidha Mhe. Nyogo amesisitiza elimu ya lishe iendelee kutolewa zaidi kwa jamii ya Watanzania, ikihusisha makundi yote muhimu, kwani bado kuna upotoshaji mkubwa unaofanyika kwenye masuala ya lishe, na wapo baadhi ya watu wanaibuka na bidhaa mbalimbali za lishe, ambazo zimekuwa na matokeo hasi kwa watumiaji na nyingine kuwaletea shida kiafya watumiaji hao.
“lazima tutoe ushauri ni chakula gani watu waweze kutumia, maana sasa hivi lishe imevamiwa kila moja ameibuka na lake, sasa kila mtu ni mtaalamu wa lishe.” Amesema Mhe. Nyongo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema wataendelea kuimarisha eneo la lishe kutokana na kuwa ni la msingi kwa Taifa, na maeneo yenye shida kwa upande wa utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe tayari yameonekana na Wizara kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na Lishe itachukua hatua za kuboresha zaidi.
Hata hivyo Dkt. Mollel ameiomba kamati ya Bunge kuangalia namna ya kuweza kuipatia nguvu Taasisi hiyo, kwani bado haina misuli ya kuweza kudhibiti baadhi ya masuala yanayoibuka kila kukicha kuhusiana na masuala ya Chakula na Lishe.
|