Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya TFNC akutana na Menejimenti

Imewekwa: 29th Mar, 2023
Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bw. Obey Assey, hivi karibuni Machi 16, 2023 amekutana na Menejimenti ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania na kufanya nao kikao cha kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Taasisi. |
![]() |
Katika kikao hicho mwenyekiti wa bodi amepata fursa ya kupitishwa kwenye taarifa za shughuli mbalimbali zinazoendelea kufanyika katika Taasisi ya Chakula na Lishe, Taarifa ambazo ziliwasilishwa na Wakurugenzi wa Idara na vitengo. |