Watumishi wa Maabara ya TFNC, wakipatiwa mafunzo ya ndani ya Mifumo ya Ubora wa Maabara

News Image

Imewekwa: 25th Jan, 2024

Watumishi wa Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, wakipatiwa mafunzo ya ndani ya Mifumo ya Ubora wa Maabara (Quality Management System) katika kutekeleza mkakati wa kuboresha huduma za maabara na kuanzisha mchakato wa kupata usajili wa Ithibati ya Ubora ISO 15189:2022 katika mwaka wa fedha 2024/25.

Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe ina ithibati ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye kupima madini joto kwenye sampuli za chumvi na mkojo na CDC IMPACT katika upimaji wa foliki ya asidi, Vit A, Vit D, Vit B12, na madini chuma.