WATUMISHI TFNC WAJITOKEZA KUPATIWA CHANJO YA UVIKO-19

News Image

Imewekwa: 5th Oct, 2021

Watumishi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) wameendelea kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kutekeleza mpango wa jamii shirikishi na harakishi dhidi ya chanjo ya UVIKO-19 baada ya baadhi yao kujitokeza kwa hiari yao kupatiwa chanjo hiyo ili kuweza kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Kabla ya kuanza kupatiwa chanjo ya UVIKO -19 watumishi hao walipatiwa semina elekezi kuhusu faida za kuchanjwa kutoka wa wataalamu wa Chanjo wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na kuondolewa hofu kuwa chanjo hizo ziko salama na zimethibitishwa na Mamlaka zinazohusika na chanjo.