Wageni kutoka Taasisi za Kimataifa wa tembelea Maabara ya TFNC

Imewekwa: 25th Feb, 2023
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania tarehe 24, Februari,2023 imetembelewa na Maafisa kutoka Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation pamoja na Chuo Kikuu cha Havard ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo katika kukabiliana na Matatizo mbalimbali ya lishe nchini.
Maafisa hao wamefika katika maabara za Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania zilizopo Mikocheni na kupokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Taasisi Bw.Obey Assey na kujionea shughuli zinazofanywa na Maabara hiyo ikiwemo za upimaji wa virutubishi mbalimbali katika vyakula.