Wageni kutoka Shirika la PANITA Tanzania na Nigeria watembelea TFNC

News Image

Imewekwa: 22nd May, 2025

Tarehe 21 Mei 2025, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), imetembelewa na wageni kutoka Shirika la PANITA Tanzania wakiongozana na wageni wengine kutoka nchini Nigeria (SUN Civil Society), ambao wamekuja kujifunza masuala mbalimbali ya kilishe chini ya mradi wa Partnership for Improved Nigeria Nutrition Systems (PINNS).

Mpango huo wa kimkakati unalenga katika kuimarisha mchango wa mashirika ya kiraia katika kusaidia upanuzi wa programu ya Multiple Micronutrient Supplementation (MMS) pamoja na kubadilishana ujuzi.

Ziara hiyo pia ililenga kukuza ushirikiano wa kina kati ya Tanzania na Nigeria katika dhamira ya pamoja ya kuendeleza matokeo ya lishe katika mataifa yote