Wafanyakazi TFNC watoa maoni na mapendekezo ya kuboresha kanuni za chakula nchini
30 Mar, 2026
Wafanyakazi TFNC watoa maoni na mapendekezo ya kuboresha kanuni za chakula nchini
Machi 27 2026, Wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) wameshiriki katika kutoa maoni na mapendekezo kuhusu Kanuni za chakula zinazoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kama sehemu ya wadau muhimu katika eneo hilo. Maoni na mapendekezo hayo yamehusisha kanuni za uuzaji na uhamasishaji wa chakula na bidhaa zilizoanishwa kwa ajili ya Watoto wachanga na wadogo za Mwaka (2026) Pamoja na kanuni ya Matangazo ya chakula na vipodozi kwa Mwaka (2026). Akizungumza wakati wa kuendesha zoezi hilo la utoaji maoni hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe Dkt. Analice Kamala, amesema maoni hayo yatawasilishwa kama maoni ya Taasisi na yataenda kusaidia kuboresha rasimu ya kanuni husika kwa kuongeza vipengele muhimu ambavyo awali vilikuwa vinakosekana kwenye kanuni ya zamani.