Wafadhili wa shughuli za lishe nchini wafanya ziara kwenye maabara ya chakula na lishe ya TFNC

Imewekwa: 26th Jun, 2023
Wafadhili wa shughuli za lishe nchini wamefanya ziara ya kikazi katika Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ili kujionea maendeleo ya upimaji wa sampuli za utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania wa Mwaka 2022 unaoendelea kufanyika katika Maabara hiyo. |
![]() |
Aidha Wafadhili hao wameridhishwa na uwezo wa Maabara hiyo katika kupima sampuli mbalimbali zinazotumika katika tafiti zinazohusiana na masuala ya chakula na lishe na pia wamepongeza uwekezaji uliofanywa na serikali katika kuboresha maabara hiyo na wametoa wito kwa wadau wa lishe kuangalia uwezekano wa kuunga mkono juhudi hizo kwa misaada zaidi na pia kutumia huduma za maabara hiyo kikamilifu. |
![]() |