07 Feb, 2026
Tarehe 3 Februari 2025, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), imetembelewa na wageni kutoka Shirika la Nutrition International Makao makuu Geneva Uswiss ili kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha mikakati ya ushirikiano katika eneo la usimamizi masuala ya lishe nchini.
Aidha, Shirika hilo pia limethibitisha dhamira yake kuendelea kuisaidia Taasisi katika utekelezaji wa jukumu lake kuu la kuongeza harakati za kitaifa za mapambano dhidhi ya aina zote Utapiamlo.
