Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya na Lishe na Mkakati na Mwongozo wa Elimu ya Afya na Lishe katika Skuli za Zanzibar

News Image

Imewekwa: 11th Dec, 2023

Leo Disemba 11, 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna, ameshiriki katika hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya na Lishe na Mkakati na Mwongozo wa Elimu ya Afya na Lishe katika Skuli za Zanzibar, Uzinduzi uliofanyika katika Hotel ya Madinal Al Bahr mjini Zanzibar.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa ripoti hiyo alikuwa Mhe. Lela Muhamed Mussa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania imeshiriki kutoa ushauri wa kitaalam kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar.Utafiti huu ni sawa na utafiti wa Malaria na Lishe (School Malaria and Nutrition Survey) uliofanyika Tanzania Bara 2019, 2021 na unaoendelea 2023.