29 Jan, 2026
Leo Januari 29, 2025 Taasisi ya Thamani Uhai kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imefanya uzinduzi wa program ya kuimarisha afya ya mama na mtoto ambayo itatekelezwa katika mikoa ya Kigoma, Geita na Katavi na eneo mojawapo litakalotekelezwa ni afua ya kuzuia na kudhibiti upungufu wa damu kwa wajawazito.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Dkt. Ahmed Makuwani, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Mama na Mtoto Wzara ya Afya kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali ambapo katika hotuba yake amesisitiza viashiria vya afya katika SDG ambapo lishe ni miongoni wa viashiria hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna ni miongoni mwa wageni walioshiriki katika uzinduzi wa program hiyo.
