Utafiti wa kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi ya chumvi yenye madini joto kuanza rasmi Zanzibar
25 Mar, 2026
Utafiti wa kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi ya chumvi yenye madini joto kuanza rasmi Zanzibar
Taasisi ya Chakula la Lishe Tanzania (TFNC), Wizara ya Afya Zanzibar, kwa kushirikiana na UNICEF na Iodine Global Network, Wanatarajia kuanza utafiti utakaoimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa Taarifa na takwimu za matumizi ya chumvi yenye madini joto kwa wanawake wajawazito katika ngazi ya jamii Zanzibar. Lengo la Utafti huo ni kuwa na mfumo endelevu wa kukusanya taarifa kutoka katika ngazi ya jamii na kusadia kufanya maamuzi sahihi katika kuzuia tatizo la Upugnufu wa madini joto. Akizungumza katika Kikao cha Kutambulisha rasmi utafiti huo kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Afya Unguja, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna, amesema Taasisi iko tayari kuto ushirikiano na msaada wa kitaalam na namna sahihi ya kufanya utafiti huu, ili kuweza kupata takwimu sahihi zinazohitajika, na zitakazosaidia kufanya maamuzi sahihi. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Salim Slim amesema kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, amepokea ujumbe huo na timu ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Taasisi pamoja na wadau wengine katika kufanikisha utekelezajki wa utafiti wa FORTIMAS. Aidha amesisitiza kutokana na madhara makubwa yanayotokana na upungufu wa madini joto kwa wanawake wajawazito, utafiti huu utaleta tija katika mapambano dhidi ya utapiamlo Zanzibar ikiwemo upungufu wa madini joto.