Utafiti wa gharama za utapiamlo (COHA) wapamba moto
Imewekwa: 10th Feb, 2024
Timu ya Taifa ya utekelezajia wa zoezi la Utafiti unaohusu gharama za Utapiamlo nchini yaani “ The Cost of Hunger in Africa -COHA ” wamekutana mkoani Morogoro kupitia na kufanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali zinazoweza kuja kutumika katika Utafiti huo ambao unaotarajiwa kukamilika Mei, 2024.
Kikao kazi hicho kimewakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Wizara ya Afya Tanzania Bara na Zanzibar,Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Kilimo Tanzania Bara na Zanzibar, Wizara ya Mifungo na Uvuvi, Ofisi ya Taifa ya Takwimu , Wizara ya Elimu, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais-Zanzibar, Taasisi za vyuo Vikuu na wadau wengine wa Maendeleo, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar.
Utafiti huu unaolenga kubainisha makadirio ya gharama zinazosababishwa na matatizo ya lishe duni/utapiamlo; kijamii na kiuchumi na hususan katika nyanja za sekta ya afya, elimu na nguvu kazi na ni utekelezaji wa maamizio ya Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kupitia mpango ujulikanao kama “The Cost of Hunger in Study in Africa- COHA)
Utafiti huo kwa hapa nchini unaongozwa na kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ambao ni Sekretarieti huku Shirika la Mpango wa Chakula Duniani ( WFP) limepewa jukumu la kutoa msaada wa kitaalam.