Umuhimu wa Mwezi wa Afya na Lishe ya Mtoto

Imewekwa: 9th Dec, 2020
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania imetoa mafunzo kwa wanahabari kutoka Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dar es salaam, Kuhusu Umuhimu wa Mwezi wa Afya na Lishe ya Mtoto, ambao unahusisha huduma za utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za Minyoo, kwa Watoto kuanzia umri wa miezi 6 hadi miaka 5.
Huduma za utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za kuzuia maambukizi ya Minyoo zimeanza kutolewa kuanzia Disemba Mosi ya Mwaka huu nchi nzima na zoezi hili litahitimishwa ifikapo Disemba 31 hivyo Mzazi au mlezi mpeleke mtoto wako mwenye umri wa kuanzia miezi 6 hadi miaka 5 katika kituo cha kutolea huduma za afya ili apatiwe huduma hii