Ulaji unaofaa kwa kuzingatia makundi matano ya vyakula

News Image

Imewekwa: 16th Jun, 2020

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imewataka wananchi kuzingatia ulaji unaofaa kwa kuzingatia makundi matano ya vyakula ili kujenga kinga ya mwili na kukabiliana na maambukizi ya magonjwa mbalimbali hususani katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugojwa wa Covid -19.

Akizungumza katika semina ya siku mbili kwa waandishi wa habari hivi karibuni, kuhusu lishe na maambukizi ya Virusi vya Corona, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Germana Leyna, amesema kwa sasa kila mtu amekuwaanazungumza lake katika ulaji wa vyakula vinavyotakiwa kuliwa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Covid-19 huku wengine wakipotosha baadhi ya matumizi ya vyakula, kuwa vina uwezo wa kutibu ugonjwa huo.

Dr Germana amesema sasa ni wakati sahihi kwa jamii kuzingatia ulaji unaofaa kwa kula makundi matano ya vyakula, ambayo ameyataka kuwa ni pamoja na vyakula vya asili ya nafaka, mizizi, ndizi mbichi, kundi la pili ni vyakula vya asili ya wanyama na jamii ya mikunde, kundi la tatu ni mbogamboga, kundi la nne ni matunda na kundi la tano ni sukari, mafuta na asali.

“Ni imani yangu jamii itapata taarifa sahihi za lishe kutoka kwenu waandishi wa habari, endapo jamii itazingatia makundi matano ya vyakula itawasaidia kupata mlo kamili,” alisema Dkt. Germana.

Kwa upande wake Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi, Bi. Hamida Mbilikila amesema mwili na kingamwili vikiwa imara vinasaidia kuzuia athari mbalimbali zinazoweza kujitokeza namaambukizi ya Covid-19.

“Mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Corona piaanashauriwa aongeze kiasi cha ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vya aina ya protini vitokanavyo na wanyama na jamii ya mikunde, vitamini na madini ,” amesema Bi. Mbilikila.

Bi. Mbilikila amesema virutubisho aina ya protini husaidia mwili kutengeneza chembe chembe au seli mpya na kukarabati seli za mwili zilizoharibika, kuimarisha mfumo wa kingamwili. Ili kupata protini, vitamini na madini kwa wingi, mtu anapaswa kula kwa wingivyakula vya asili ya wanyama, mboga mboga na matunda.

Nae Afisa Lishe Mtafiti wa Taasisi hiyo , Bi. Fatma Mwasora akizungumzia lishe kwa wanawake wajawazito nawanaonyonyesha katika kipindi cha ugonjwa wa Covid-19 amesema wanapaswa kula mlo kamili unaotokana na vyakula mchanganyiko mara nne hadi tano kwa siku.

Akifafanua kuhusu maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, Bi. Fatma amesema hadi sasa hakuna utafiti wowote uliothibitisha kwamba virusi vya Corona vinaweza kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa unyonyeshaji.

Akizungumzia kuhusu matumizi ya matunda na viungo katika kupambana na dalili za maambukizi ya virusi vya Corona, Afisa Mtafiti wa TFNC, Bi. Victoria Kariathiamesema jamii inapaswa kuzingatiakutumia matunda yenye vitamini C kwa wingi, mdalasini, tangawizi, kitungu saumu na mchaichai, kwani matunda hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuondoa dalili zinazoambatana na ugonjwa huo.