Ukiliona kituoni usisite kupanda

News Image

Imewekwa: 9th Jun, 2024

Mkazi wa Dar es Salaam, Mbeya na Unguja Zanzibar, Ukikutana na Daladala hii kwenye kituo chako usisite kulipanda, Utaenda nalo hadi mwisho wa safari yako huku ukipata elimu juu ya matumizi sahihi ya vyakula vinavyotuzunguka na kuhamasisha ulaji unaofaa kwa kila mmoja wetu, ili kuweza kupunguza matatizo ya kilishe miongoni mwa Watanzania.


Ukiwa ndani ya Daladala hii elimu utakayopatiwa itazingatia Mwongozo wa Taifa wa Chakula na Ulaji Sahihi ambao umezingatia uwepo na matumizi ya vyakula vya asili vilivyopo katika mazingira yetu, na kuelekeza vipimo sahihi kwa kila mlo au chakula na kinywaji ambacho binadamu anatakiwa kupata kwa siku.

Elimu itakayotolewa kwa njia ya usafiri wa daladala itazingatia Mwongozo wa Taifa wa Chakula na Ulaji Sahihi ambapo umezingatia uwepo wa matumizi ya vyakula vya asili vilivyopo katika mazingira yetu, na kuelekeza vipimo sahihi kwa kila mlo au chakula ambacho binadamu anatakiwa kupata kwa siku.

Kampeni hii pia imehusisha Taasisi nyingine zisizo za Kiserikali ikiwemo Nutrition Connect Tanzania pamoja na Tanzania Girl Guide Association ambapo mbali na kutekelezwa katika Mkoa wa Dar es Salaam pia itafanyika katika Mkoa wa Mbeya na Unguja Zanzibar.