Ujumbe wa wataalamu kutoka msumbiji watembelea maabara ya chakula na lishe ya TFNC
27 Oct, 2025
Ujumbe wa wataalamu kutoka msumbiji watembelea maabara ya chakula na lishe ya TFNC
Oktoba 09, 2025 Ujumbe wa wataalamu wa kutoka Chuo Kikuu cha Eduardo Mondlane, Wizara ya Uchumi na Wizara ya Afya kutoka nchini Msumbiji, umefanya ziara ya kutembelea maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) iliyopo Mikocheni jijini Dar es salaam ili kujifunza namna inavyofanya kazi zake katika uchambuzi wa sampuli mbalimbali za vyakula na zile za kibaolojia. Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ni maabara rejea kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na kati na Kusini, na matokeo ya uchunguzi wa viashiria vya hali ya lishe na virutubishi yanayotolewa na maabara hii, yanaaminika kimataifa (WHO, CDC, ECSA-HS, IGAD), na kuifanya kuwa maabara pekee ya lishe inayoaminika ukanda huu.   Wataalamu wa Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), wakiendelea na uchunguzi wa kimaabara kwenye sampuli za chakula zinazoletwa kwenye Maabara ya Chakula na Lishe , kwa ajili ya kuangalia aina na kiasi cha virutubishi vilivyomo kwenye sampuli hizo. Ujumbe wa wataalamu wa kutoka Chuo Kikuu cha Eduardo Mondlane, Wizara ya Uchumi na Wizara ya Afya kutoka nchini Msumbiji, umefanya ziara ya kutembelea maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) iliyopo Mikocheni jijini Dar es salaam ili kujifunza namna inavyofanya kazi zake katika uchambuzi wa sampuli mbalimbali za vyakula na zile za kibaolojia. Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni; • Kemia ya Chakula –Inahusika na Uchunguzi wa viinilishe, uchafuzi na sumu za asili mfano sumukuvu, cyanide kwenye mihogo n.k • Biokemia- Inahusika na uchunguzi wa viashiria vya lishe mwilini na hali ya lishe • Mikrobiolojia- Inahusika na uchunguzi wa viashiria vya viini lishe mwilini na uchunguzi wa ubora na usalama wa chakula.